Sunday, September 16, 2012

THEA YUKO MBIONI KUACHIA FILAMU MPYA YA "MALAIKA WANGU"


Msanii wa filamu bongo anayefanya vizuri Thea, ameuambia mtandao huu kuwa hivi karibuni anatarajia kutoa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina ‘Malaika Wangu’, ambayo kwa sasa ipo kwenye hatua za mwisho za editing.

Alisema kuwa filamu yake mpya ni kazi ambayo imefanyika kwa umakini mkubwa na wasanii wote waliocheza katika filamu hiyo wote wameonesha kiwango cha hali ya juu.


“Nakata kuwafahamisha mashabiki wangu kuwa mzigo mpya unakaribia kuingia sokoni, wategemee kazi nzuri na pia nawasihi watanzania wapende  kununua kazi original sio feki ili kusapoti tasnia ya filamu nchini”
alisema.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!