Monday, September 3, 2012

UGONJWA WA MOYO WAMTESA BEBE COOL NA KUMFANYA ASITISHE ZIARA YAKE

Mwanamuziki wa Uganda Bebe Cool anasumbuliwa na maradhi ya moyo ambayo yamemlazimisha kusitisha ziara yake ya hivi karibuni.

Tatizo lake la moyo lilianza baada ya kupigwa risasi mwaka 2010 kwenye super market ya Nakumatt jijini Kampala, ambapo tangu hapo amekuwa na matatizo makubwa ikiwa pamoja na kusumbuliwa na ndoto za kutisha.

Hivi karibuni alipata mshtuko mbaya wa moyo nchini  Canada. Kutokana na matatizo  hayo, imeripotiwa kuwa  hatoweza kufanya ziara yake nchni Marekani.

Kutokana na tukio hilo la kupigwa risasi Bebe Cool anaitaka serikali imlipe shilingi bilioni 2.9 za Uganda.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!