Friday, September 7, 2012

ULIDHANI NI SIFA KUOA WAWILI? ...PENTAGON ATANGAZA KUWATIMUA WAKE ZAKE BAADA YA KUSHINDWA "KUWAHUDUMIA"Wake zake Pentagon, Baby Mai na Rahma.

MUIMBAJI wa Bendi ya Extra Bongo, Ramadhan Mhoza ‘Pentagon’ amefunguka kuwa amechoshwa na wake zake hivyo hana muda mrefu atawatimua wote ili aishi peke yake.


Akiongea  a  mwandishi wetu, Pentagon alisema awali alidhani kuwaoa wanawake hao ambao ni Baby Mai na Rahma wangemuongezea furaha katika maisha yake lakini matokeo yake wanamtia kichaa.

Ramadhan Mhoza ‘Pentagon’.
Alisema kitu kikubwa kinachomfanya afikirie uamuzi huo ni wivu uliopitiliza hadi kuwa kero kwake na kumfanya ashindwe kufanya mambo yake kiufasaha.

 “Nimeamini kweli wanawake ni pasua kichwa kwani wanaoneana wivu wa kijinga wanabaki kuniumiza kichwa tu mimi, kuanzia mwezi ujao naanza kuishi singo, nitaondoka nyumbani nikatafute sehemu niishi peke yangu nitulie kimya,”
alisema Pentagon.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!