Wednesday, September 12, 2012

VIBAKA WAMLIZA WEMA SEPETU BAADA YA KUKOMBA VIOO VYA GARI LAKE


Wema Isaac Sepetu, hivi karibuni alijikuta akipata wakati mgumu baada ya kukombwa vioo vya gari lake aina ya Toyota Mark X  na vibaka wa Moshi, Kilimanjaro

Tukio hilo limetokea hivi karibuni ndani ya Viwanja vya Chuo cha Ushirika  ambapo staa huyo alikuwa amehudhuria uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.


Akiwa katika burudani hizo, Wema  ambaye muda mwingi alionekana kuwa mtu mwenye furaha ghafla alibadilika na kuishiwa na furaha alipolikuta gari lake likiwa limekongolewa vioo vyote vya pembeni.

Mtandao  huu ulizungumza na  Wema  kuhusu tukio hilo ambaye alionekana  kushangazwa  na tukio hilo na kusema kuwa  hakutarajia  kukutana nalo  kwa kuwa alikuwa  akiwaheshimu sana watu wa Moshi.

“Imeniuma sana baada ya kukuta gari langu limekongolewa,  wameiba vioo na ukiangalia nipo ugenini, halafu magari ni mengi yaliyokuwa yamepaki uwanjani, kwa nini yasiibiwe hayo mengine wakaiba langu tu, dah! imenikera sana,” alisema Wema kwa uchungu. 


Hilo ni tukio lingine la Wema kulizwa, alishawahi kuibiwa nyumbani Sinza jijini Dar baada ya wezi kuruka ukuta na kumkomba baadhi ya vitu vya thamani, pia alishawahi kuibiwa vitu vingine ndani ya gari Uwanja wa Taifa.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!