Tuesday, September 11, 2012

"BENJAMIN WA MAMBO JAMBO" KUJA NA NGOMA MPYA ALIYOIPA JINA ‘SKENDO’


MSANII anayepagawisha mashabiki wengi kutokana na sauti yake ‘Benjamini wa Mambo Jamo’, ameuambia mtandao huu kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Skendo’, ambayo itazungumzia namna watu wanavyitengenezea skendo kwa lengo la kujipatia umaarufu usiyo na maana.

Akizungumza na mwandishi wetu 
, alisema kuwa ngoma hiyo inakuja hivi soon na ipo katika mtiririko mzuri wa mashairi pamoja na ujumbe wake, kitu ambacho kinaashiria kuwa itafanya vizuri kwani kwa upande wake si msanii ambaye anatoa ngoma kila baada ya wiki mbili.

Msanii huyo aliwahi kutamba sana na ngoma ya yake ya 
‘My Friend’, ambayo inazungumzia mambo mengi ya maisha na njisi ndugu yako anavyoweza kukumaliza kwa ajili ya pesa au kutaka kuwa juu ya yako.

“Mimi si msanii ambaye anatoa ngoma kila baada ya wiki kwani najua kusoma alama za nyakati hivyo napokuwa kimya huwa natafakari ni namna gani naweza kutoa kitu kizuri kwa ajili ya mashabiki wangu,”
alisema.

Hata hivyo sasa msanii huyo ana kampuni yake ya kutengeneza video inayoitwa
Promo Only ambapo pia matarajiao yake ni kuwa na kampuni kubwa zaidi ya atakayoipa jina la B.M.L, ambayo itahusika zaidi na video pamoja na audio.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!