Monday, September 24, 2012

WAFANYAKAZI WA EATV WAJITOSA NA KUTEMBEA JUU YA MOTO


Uanaume wa shoka
Wafanyakazi wa East Africa TV juzi walilazimika kutembea juu ya moto kama ishara kuwa wanaweza kukabaliana na changamoto zozote wanazokutana nazo mbele.

Zoezi hilo limefanyika baada ya kupewa semina ya siku mbili kutoka kwa wahamasishaji wa Peak Perfomance.

“Kutembea juu ya moto ilikuwa ni kuhamasisha moyo wa kujiamini na kuthubutu. Walilenga kumpa kila mtu morale ya kujitambua kuwa ana uwezo wa kufanya kitu unachohofia kuwa huenda huwezi kujichanganya,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa EATV.

Unaweza kutembea juu ya moto?
Uanaume wa shokaCameraman wa EATV, Ombeni akimaliza zamu yakeDada upande wa kushoto maumivu yalimwelemeaHakuna kuremba (600x800)
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!