Wednesday, September 26, 2012

“WANAWAKE WA BONGO MOVIE WANAPENDA KUMEGWA NA WANAUME WANAOUZA MADAWA YA KULEVYA WAKIDHANI WATATAJIRIKA ” – SHILOLE…!!

WAKATI wasanii wengi wakishindana kwa kubadilisha magari ya kifahari hapa mjini, msanii wa filamu na muziki Shilole, amefunguka na kudai kuwa kuna kasoro kubwa hasa ya kiumaskini kwani wanawake wengi wa bongo movie wanapenda kumegwa na wanaume wanaofanya biashara haramu ya madawa ya kulevya kwa kudhani kuwa watapewa dili la kulala maskini na kuamka tajiri.

Wapo wasanii wengi ambao wanajisifu kwa kuwa na magari ya kifahari lakini ukitazama kwa hali ya kawaida gari analiotembelea na thamani ya hela anayolipwa katika kila filamu wala haviendani.


Shilole
alidai kuwa kasoro hiyo inasababishwa na tamaa za baadhi ya wasanii kwani wanaamini wakitembea na wanaume wanaofanya biashara hizo nao wanaweza kufanikiwa mapema huku wakisahau kuwa riziki hutoa Mungu na si binadamu yeyote yule.

Msanii huyo alidai kuwa wapo baadhi ya wasanii ambao wamefanikiwa si kwa kuwatengemea wanaume, lakini asilimia kubwa wanakaa na kujipendezesha wakisubiri mwanaume ndiye wawafanyie kila kitu eti kwa sababu ya umaarufu wao.


“Hata siku moja uji kusikia eti Shilole anaishi mjini kwa sababu mtu ya fulani .Mi ni jembe nimekuja mjini kutafuta na si kutafutiwa kama wasanii wengine wanasubiri kupata mwanaume anayefanya biashara harumu ili nao wamepewe dili la kulala maskini na kuamka na tajiri,”
alidai.

Hata hivyo aliongeza kuwa wanawake wengi wanatumia miili yao kama sehemu moja wapo ya kujiigizia kipato huku wakisahau kuwa kuna magonjwa hatari kama Ukimwi na mengine mengi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!