Monday, September 10, 2012

WASANII WAFUNGUKA KUHUSIANA NA KIINGEREZA KAMA KINACHANGIA UKUAJI WA MUZIKI NCHINI

AFANDE SELE
Muziki ni hisia ndio maana hata baadhi ya watu wanapenda miziki ya kihindi au kilatini bila kujua maana kutokana na hisia zao kutekwa na jinsi waimbaji walivyowasilisha hisia kupitia muziki. 

Hivyo mie nadhani lugha sio tatizo kubwa kwa muziki wetu kuweza kwenda level ya kimataifa, tunachohitaji ni kuwa utambulisho wa muziki wa kitanzania ambao msanii yoyote haijalishi awe anachana au kuimba akitoa tu ngoma yake ijulikane hii ni kutoka Tanzania.

MARCO CHALI
Language sio kigezo kabisa kwani muziki wa kizaire umefika mbali sana na hakuna anaelewa. 

Hivyo  ni ubunifu na wasanii na maproducer kuwa serious kufanya muziki uwe biashara. Then kila kitu kitakuwa poa na international market itakuwa real, mbona Diamond, Kiba wanapiga show na hiki hiki kiswahili na wanakubalika.

SOLO THANG
Nadhani lugha ni tatizo lakini sio kubwa kihivyo. Unaposema lugha ni tatizo ya muziki wetu kupenya nje ya mipaka yetu vipi kuhusu Cabo Snoop ambaye anaimba kireno na naamini ni watu wachache sana ndio wanamuelewa lakini bado wanampenda na amefanikiwa. So its all about identity ya muziki.

MANECK
Tatizo sio language ni uvivu wa kuumiza kichwa wasanii wengi wanataka kutumia kivuli cha wasanii wengine. 

Kila anayekuja sasa hivi anataka kutambaa mwendo wa msanii flani, nadhani ndiyo kikwazo kikubwa cha mziki wetu kutokufika mbali.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!