Saturday, September 22, 2012

WEASEL NA RADIO WAKAMATWA KWA KUINGIZA BIDHAA BILA KULIPIA KODIMaswahiba wa kundi la Goodlyfe la nchini Uganda, Radio na Weasel wiki iliyopita walimakatwa na walinzi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe baada ya kuingiza bidhaa ambazo zilikuwa hazijalipiwa kodi.

Wawili hao walikuwa wakitokea nchini China wakiwa na suitcase zilizokuwa zimejaa simu, nguo na viatu ambavyo vilikuwa havijakaguliwa kwenye ofisi za custom.

Inadaiwa kuwa wasanii hao waliomba msamaha na kuahidi kutorudia tena na ndipo walipoachiwa.

Hata hivyo walilazimika kulipa faini ya shilingi milioni sita za Uganda kama nusu ya kodi waliyotakiwa kulipa.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!