Wednesday, October 31, 2012

"DIAMOND AMEIBA ISEA YANGU NA ANATUMA WATU ILI WAIBE FLASH YENYE HUO WIMBO"....H.BABAScandal inayohusiana na wimbo mpya wa Diamond ‘Nataka Kulewa’ imeendelea kuchukua sura mpya baada ya H.Baba leo kuuambia mtandao huu kuwa Diamond Platnumz ameanza kutuma watu wake ili waiibe flash yenye wimbo wake (H baba) ili kusiwepo ushahidi.

“Ninayo kwenye flash lakini siwezi kuiacha sehemu yoyote sababu ameshatengeneza mpaka watu waibe hii flash, yaani sasa ni michongo tu ya ajabu ajabu inaendelea sasa hivi,” amesema.

‘Kwasababu kule studio yaani verse zote zimefutika lakini mimi nilikuwa nayo kwenye flash yaani ile demo nilichukua kwaajili ya kusikiliza nyumbani, studio verse zote zimepotea, huwezi amini.”

Amesema hana lengo la kuuachia wimbo huo lakini atatoa kipande kifupi ili watu wasikie kile anachokisema.

Msanii huyo anasema Diamond alimkuta kwenye studio ya G Records wakifanya wimbo wenye jina hilo (Nataka Kulewa) ambapo Q-Chief aliimba chorus na Diamond kuusifia sana.
Msikilize zaidi hapa:

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!