Wednesday, October 3, 2012

AMINA MOLLEL AILILIA KITCHEN PARTY YAKE...


MTANGAZAJI maarufu Bongo anayepiga mzigo katika Runinga ya TBC 1, Amina Mollel  ameangua kilio cha furaha katika sherehe yake ya kufundwa maarufu zaidi kwa jina la Kitchen Party, ikiwa ni maandalizi ya ndoa yake.

Tukio hilo limetokea katikati ya wiki iliyopita katika Ukumbi wa Next Door, Tabata jijini Dar es Salaam ambapo ilihudhuriwa na watu wengi maarufu na wasio na majina.

Katika kuonesha tofauti, Amina aliingia ukumbini humo akiongozana na wapambe wake ambapo wote walikuwa wamevaa mavazi ya Kimasai, huku mtangazaji huyo akiwa ameshika fimbo mkononi mwake.


Malkia wa mipasho Afrika Mashariki, Khadija Kopa alitinga ukumbini humo na kuimba nyimbo zake ambazo wanawake wengi wanazipenda,  kitendo kilichowainua waalikwa na kuanza kucheza naye.

Baada Khadija kupagawisha, Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ walivamia jukwaa na kukonga nyoyo za mashabiki kwa sebene safi.

 “Ni siku niliyokuwa naisubiri kwa hamu kubwa. Siamini hata kidogo. Najisikia furaha sana na kila ninayemuona hapa anazidi kuniongezea furaha ya ajabu moyoni mwangu, ndiyo maana nashindwa kuyazuia machozi yangu,” alisema Amina.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!