Saturday, October 13, 2012

AUNT LULU ATOWEKA KWAO NA KUHAMIA GESTI


MWANADADA asiyeishiwa na matukio, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ anadaiwa kutoroka kwao na kwenda kuishi gesti ikiwa ni siku chache baada ya kutimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa anaishi.

Chanzo chetu cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, Lulu tangu atimuliwe kwenye nyumba aliyokuwa anaishi alikaa kwao maeneo ya Tabata kwa siku chache tu kisha akaenda kuishi gesti na marafiki zake.

 
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alikwenda hadi kwenye gesti hiyo iitwayo Samit lakini hakufanikiwa kumkuta msanii huyo na alipompigia simu na kumuuliza juu ya madai hayo alisema:


 “Jamani mimi naishi pale na marafiki zangu ambao nimeshawazoea ila ni kwa muda wakati najipanga na kiukweli hata ndugu zangu hawajui kama nipo hapa,” alisema Aunty Lulu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!