Tuesday, October 2, 2012

BAADA YA KUTOSWA KWA MIAKA MITANO MFULULIZO, HATIMAYE T.I.D APATA SHAVU LA KUPERFORM FIESTA YA DAR
Baada ya miaka mitano bila kupata nafasi ya kupanda kwenye stage ya show za Fiesta, hatimaye Top in Dar, TID, atapanda kwenye show ya kilele cha tamasha hilo la kila mwaka, litakalofanyika October 6 kwenye viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam.

Hiyo inamaanisha kuwa TID ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akijiita ‘Mnyama’ atashare stage moja na Rick Ross.

”KinoNdoNi+Fiesta+MnYaMA is equal to ‘Mtama wa ShiNGo’…..BhaaaaS Watoto WadoGo mmekWiShA", ameandika TID ambaye jina lake ni Khalid Mohamed kupitia Facebook.

Kupitia XXL ya Clouds FM, watangazaji wa kipindi hicho wamesikika wakimtaja TID kama msanii rasmi atakayetumbuiza kwenye show hiyo.

Hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Facebook, hitmaker huyo wa ‘Kiuno’ alitoa malalamiko yake kwa kutokuhusishwa kwenye show hiyo kwa muda mrefu.

“I wiSh I coUld maKe the Guy Who does the FieSta Listing be oN my SiDe some PeoplE are workin verY Hard to juSt makE me Look like Criminal so I can not be on List Lakini Mungu atanipa Better than Fiesta tho its Been 5 years am nt Part of It,” aliandika.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!