Thursday, October 18, 2012

"NILIKUWA BIZE NA MAMBO YANGU NA NDO MAANA SIKUHUDHURIA PARTY YA KUVISHWA PETE FROLA MVUNGI ".....NISHA


WAKATI staa wa bongo movie Frola Mvungi, akiwa amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake H-Baba, msanii mwenzake Salma Jabu ‘Nisha’, amefunguka na kudai kuwa aliamua kutokwenda kwenye party ya msanii huyo na si kwamba anamuonea wivu bali alikuwa bize
na mambo yake pamja na hayo hakupewa mualiko.

Akiongea na Mwandishi wetu 
  kuhusu ishu hiyo, Nisha alidai kuwa watu wanaodaiwa kuwa anamuonea wivu Mvungi wanamtafuta maneno kwani hajawahi kuchukiana na rafiki yake huyo na mara zote huwa wanafanya kazi pamoja na hawawezi kukwaruzana kwa sababu ya pete.

“Jamani kwanza sikupewa taarifa kuwa anavishwa pete na hata hivyo nilikuwa bize na kazi zangu, lakini mbali ya yote sina bifu na Mvungi na tunafanya kazi pamoja kila siku,”
alidai.

Mvungi
naye alipotafutwa ili kueleza ni kwanini hakumpa mualiko mwezake alidai kuwa hata yeye hakujua kama anavishwa pete na wale wachache waliokuwepo walitosha kwani haikuwa na watu wengi kiasi kwamba Nisha aanze kulalamika.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!