Wednesday, October 10, 2012

"NAMPENDA BWANA MISOSI KWA SABABU HANA DHARAU NA ANAJIHESHIMU".....AMANDA

MSANII wa Filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka  kuwa heshima aliyonayo staa wa Muziki wa Bongo fleva, Joseph Lushalu `Bwana Misosi’ ndiyo iliyomfanya ampe penzi lake.

Akiongea na mwandishi wa habar hii, Amanda alisema yeye siyo kama wanawake wengine ambao wanavutiwa na sauti,swaga na  sura, bali amempenda Bwana Misosi kutokana na heshima aliyonayo katika jamii.
 

“Bwana Misosi hana dharau, anawaheshimu wakubwa na wadogo pia ana mapenzi ya dhati tofauti na wanaume wengine wa siku hizi,” alisema.

Aidha, alisema kuwa kutokana na hivyo anampenda mpenzi wake huyo kuliko kitu chochote na anamuomba Mungu ayaendeleze  mapenzi yao ya dhati ili wadumu milele.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!