Saturday, October 6, 2012

CHRIS BROWN AWA DIAMOND WA BONGO...."NASHINDWA NANI NIMUACHE KATI YA KARRUECHE NA RIHANNA"Rihanna & Chris Brown
Muda mchache baada ya Chris Brown kutangaza kumuacha girl friend wake Karruache eti kwa sababu ya urafiki wake na Rihanna na pia hakutaka kuendelea kumuumiza mrembo huyo, sasa mambo yamekuwa tofauti.

 Chris B ameamua kutoa ya moyoni na kusema bado anawapenda sana wote wawili na anashindwa kabisa afanye nini.

Katika clip ya video iliyowekwa kwenye mtandao inamuonesha Chris Breezy akifunguka “ nashindwa kupata the really Chris Brown, sasa nataka kuwa mkweli. I’m just stressed out.

 Sio kwa sababu ya muziki, nawapenda mashabiki wangu, ni vile unavyoshare historia na mtu halafu unaanzisha mahusiano ya mapenzi na mtu mwingine, inakuwa ngumu…hivi kuna kitu kama kuwapenda watu wawili? Sijui kama inawezekana, lakini hivyo ndivyo ninafeel.”

Mskilize Chris mwenyewe hapa:
Hii inaonesha wazi kuwa anawapenda wote kwa wakati mmoja, na sio kama alivyosema kuwa Rihanna ni rafiki yake tu ambae amepelekea amuache girl friend wake ili asiuharibu urafiki wao.

Rihanna na Chris Brown wameshindwa kuficha feeling zao kabisa, mbali na kuwepo kwa rumors kuwa walikuwa wanawasiliana mara kwa mara, wali kiss wakati wa MTV VMAs, lakini hivi karibuni Rihanna alitweet na kumuita Chris ‘baby’ akim-wish all the best alipokuwa anaenda mahakamani, na inasemekana wivu wa Karrueche haukujificha katika hili, hakupenda kabisa.

Hivi karibuni watatu hao walikutana Brooklyn walipokuwa wameenda katika tamasha la Jay-Z, na Chris Brizzy alikaa na Rihanna katika hotel aliyofikia Rihanna kwa muda wakati Karruache akimsubiri Chris room walipofikia kwa muda wote huo, na tweets nyingi za kushangaa kile alichokuwa akifanya Chris alizipata Karrueche na naamini hiki ndicho kilichomuumiza sana mrembo huyu.

Ukiacha mbali hayo yote aliyokuwa anafanya Chris na Rihanna, wakati wanaelekea Baclay Center mida ya saa mbili za usiku kwa saa za huko marekani, Karrueche alitweet ‘Bye Baby”, duh..huyu mrembo kweli amependa.

Nadhani huu moyo ndio unamfanya Chris awe katika dilemma,japo alitangaza rasmi kuwa amemuacha Karruache ili asimuumize kutokana na huu urafiki wake na Rihanna, sasa ameamua kusema  anawapenda wote, ila haiwezekani kuwapenda watu wawili kwa wakati mmoja na kuwa-satisfy wote.

Hapa lazima atachaguliwa mmoja, nani hasa atapewa moyo wote wa Chris, tusubiri vitendo tutapata majibu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!