Friday, October 5, 2012

DITTO ASHINDWA KUWIKA KWENYE TUZO ZA RFI.....MNAMIBIA ABEBA USHINDI


Elemotho Gaalelekwe
Msanii wa THT Lameck Ditto ameshindwa kutamba kwenye tuzo za the RFI France 24 Discoveries Awards 2012 alizokuwa ametajwa kuwania.

Mwanamuziki wa nchini Namibia Elemotho Gaalelekwe ndiye aliyeibuka mshindi.


Wasanii wengine waliokuwa wakiwania tuzo hizo ni pamoja na Maryse Ngalula (DRC), Spyrow (Cote d’Ivoire), Denis Larose (Mauritius), GT the Guitarman (Nigeria), Tafeifa (Senegal), Nasser (Mauritania) na Trio Teriba (Benin).

Mshindi huyo atazawadiwa kiticha cha €10 000, kupewa promotion, kutumbuiza kwenye tamasha kubwa mjini Paris Ufaransa na ziara barani Afrika.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!