Wednesday, October 24, 2012

"DIAMOND HANA UHUSIANO NA NAJMA"......HII NI KAULI YA MENEJA WA DIAMOND


Najma na Diamond
Kumekuwepo na tetesi za chini kwa chini kuwa Diamond na aliyewahi kuwa mpenzi wa Mr Blue, Najma ni wapenzi. 

Tetesi hizo zilipamba moto baada ya kuonekana kwa picha za birthday za Diamond ambapo Najma alikuwa miongoni mwa waalikwa.
Hata hivyo kwa mujibu wa meneja wa Najma ambaye kwa muda mrefu alikuwa nchini Uingereza kimasomo, mastaa hao wako karibu kikazi zaidi tu na hakuna kingine.

“Mimi niliamua Najma afanye nyimbo na Diamond nikamuomba Diamod,Diamond akakubali kwahiyo tuna project na Diamond all time tunakuwa na Diamond kwasababu ni project ambayo tunataka kufanya nae, lakini this time as a friend lakini si kama wapenzi,” Meneja wa Najma aitwaye Nasra ameimbiwa Power Jams ya EA Radio.
“I think watu wamekuwa confused kwasababu kila tukiwa na Diamond picha nini na nini tunaweka BBM so wanakuwa wanapata ile confusion ,sasa ni kazi kama kazi nyingine kama watu wanavyofanya na watu.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!