Thursday, October 11, 2012

HATIMAYE FROLA MVUNGI NA H. BABA WAVISHA PETE YA UCHUMBA


MWIGIZAJI zao la mchezo wa Bongo Dar es Salaam, Flora Mvungi amevishwa pete ya uchumba na Hamis Baba ‘H-Baba’ baada ya kuishi kinyumba na mwanaume huyo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Akiongea  na mwandishi  wa habari hii, Flora alisema safari yao ya kuelekea kuoana na H-Baba ilipigwa vita na wengi lakini kwa sasa anamshukuru Mungu dalili za ndoa zinanukia.

“Kuna baadhi ya ndugu waliweka pingamizi mimi na H-Baba kufikia hatua hii, nilisubiri sana, hatimaye jamaa kaleta posa nyumbani na kanivisha pete ya uchumba,” alisema Flora.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!