Wednesday, October 24, 2012

HATIMAYE H.BABA AMLIPIA MAHALI FROLA MVUNGI

ULE uchumba uliodumu kwa muda mrefu kati ya mastaa filamu na muziki wa Bongo Fleva nchini, Hamis Baba ‘H. Baba’ na Flora Mvungi umefikia pazuri baada ya H – Baba kumtolea mahari na kumvalisha pete ya uchumba.

H-Baba akimvisha pete ya uchumba, Flora Mvungi.
Tukio hilo lililokuwa na mvuto wa aina yake lilichukua nafasi juzi Jumamosi, katika Ukumbi wa The Atriums Hotel, Sinza – Afrika Sana, Dar na kuhudhuriwa na ndugu wa pande zote mbili.


Kinyume na ilivyozoeleka, zoezi la kutoa mahari kufanyika nyumbani, kwa wawili hawa ilikuwa tofauti kwani kila kitu kilimalizikia ukumbini humo.

H-Baba akiwasalimiana ndugu na jamaa.
Kwanza lilianza zoezi la makabidhiano ya mahari, kisha ndipo H – Baba akaruhusiwa kumvalisha Flora pete ya uchumba, tendo lililoamsha shangwe na vigelegele ukumbini humo.

Flora Mvungi kabla ya kuvishwa pete ya uchumba.

“Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kufanikisha tukio hili, japokuwa gharama ilikuwa kubwa lakini niliweza kujitutumua mwenyewe bila kuomba mchango kwa mtu yoyote.....Alisema H baba  na kuongeza:


“Jambo kubwa ninalotamani litokee na ninaamini litafanikiwa ni kufunga ndoa na Flora wangu. Ninampenda sana na nina uhakika na uchaguzi wangu.”H-BABABaadhi ya mastaa waliohudhuria ni pamoja na Baby Madaha, Kulwa Kikumba ‘Dude’,  Hisani Muya ‘Tino’, Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Husna Idi ‘Sajenti’ na Wilson Makubi aliye Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).

Ndugu na jamaa waliohudhuria tukio hilo.
H-Baba akiwasalimia wageni waalikwa.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!