Tuesday, October 2, 2012

"POMBE ILINIFANYA NIWE KIKOJOZI".....BABY MADAHA


STAA wa filamu na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ameweka wazi  kuwa suala la udokozi wa pombe alipokuwa mdogo, ndilo lilipelekea awe kikojozi.

Akifunguka mbele ya Mwandishi , Baby Madaha alisema kipindi anasoma shule ya msingi alikuwa akiiba pombe kwenye friji nyumbani na kubugia hivyo kumfanya ashindwe kujizuia usiku na kujikuta anakuwa kikojozi.

“Dah! Mama alikuwa anakasirika sana, ananichapa kishenzi bila kujua sababu kuwa ni pombe,” alisema Baby Madaha.

gpl
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!