Monday, October 8, 2012

JACK WOLPER AJIPANGA KUTOKA NA" AFTER DEATH " YENYE LENGO LA KUMUENZI KANUMBAMuigizaji wa kike wa Bongo Movies Jackline Wolper yupo location kushoot filamu yake mpya iitwayo ‘After Death’ anayoigiza na watoto wawili waliowahi kuigiza na marehemu Steven Kanumba kwenye filamu zake za ‘Uncle JJ’ na ‘This is It’ Jennifer na Patrick.
Jennifer akipokea tuzo zilizotolewa na mtandao wa filamucentral
Akiongea na Movie Leo ya Clouds FM, Jackline amesema ameamua kufanya filamu hiyo kama njia ya kumuenzi kutokana na kuwa na mchango mkubwa kwenye career yake ya filamu.

Amesema baada ya kifo cha Kanumba, aliwaahidi watoto hao kuwa ataendeleza vipaji vyao vya uigizaji kwakuwa Kanumba alikuwa kama baba yao.

Jackline amesema After Death itashirikisha wasanii wengine kama Shamsa Ford, Mariam, Pancho Mwamba na wengine.
Ameongeza kuwa kwenye filamu hiyo amemtumia mtu ambaye anafanana sana na Kanumba ili kuifanya story iendane naye.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!