Wednesday, October 31, 2012

JB NA BANANA ZORRO WAPAMBANA KWENYE "UKURASA MPYA"

Ile filamu ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu sasa ipo madukani tangu siku ya jana.

 Filamu hii inamuhususisha nguli wa filamu kwa sasa ambaye amejizolea mashabiki wengi kutokana na movie anazozitoa zikiwa na story nzuri kumpelekea shabiki kufurahia pesa yake aliyotoa kununua movie zake.Si mwingine ni Jacob Stephen alias JB.

Kupitia kampuni yake ya A Jerusalem Film, JB ameweza kutengeneza movie hiyo ambayo sasa imeingia sokoni na inasambazwa na kampuni ya Steps Entertainment LTD

 Katika movie hii ya “Ukurasa Mpya” utapata nafasi ya kumuona mkali wa Muziki wa Bongo Flavour ambaye anamiliki bendi ya B-Band, Banana Zorro ambaye sasa amekuwa anaonyesha uwezo mkubwa katika kuigiza, Pia utapata nafasi ya kumuona mchekeshaji mkali Soudy Ally.

Hii ni movie ya pili kwa JB kuigiza na Banana Zorro, baada ya ile ya kwanza iliyokuwa inaitwa D.N.A ambayo Banana alionyesha uwezo mkubwa alivyo Act kama Doctor.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!