Wednesday, October 31, 2012

LORD EYEZ APELEKWA MAHAKAMANI LAKINI ASHINDWA KUPANDISHWA KIZIMBANI


Rapper wa kundi la Weusi Lord Eyez leo asubuhi alifikishwa mahakamani katika mahakama ya wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaa akitokea mahabusu katika kituo cha polisi cha Oysterbay na kushindwa kupanda kizimbani baada ya hati ya mashtaka kutokidhi mahitaji ya kisheria.

Lord Eyez alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi katika defender, chini ya ulinzi mkali wa polisi na kupelekwa moja kwa moja mahabusu akifichwa asionekane hadharani kwa waandishi wa habari ambao walijazana kwa wingi katika eneo la mahakama hiyo.

Aidha, shauku ya watu wote waliokuwepo mahala hapo ilipotea pale walipopata taarifa kwamba msanii huyo hatapandishwa mahakamani kwa kuwa hati yake ya mashataka ilikuwa na makosa tofauti na anayotuhumiwa nayo, hivyo kuhitajika kufanyiwa marekebisho kabla ya kupelekwa kwa mwanasheria mkuu na kurudishwa mahakamani kwa ajili ya kupangiwa siku ya msanii huyo kufikishwa mahakamani tena.

Kutokana na ulinzi mkali, ilikuwa ngumu kupata picha zake.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!