Saturday, October 27, 2012

LUCY KOMBA APATA SHAVU LA KUFANYA FILAMU NCHINI DENMARK


 
STAA wa sinema za Bongo, Lucy Francis Komba amekula shavu la kufanya filamu nchini Denmark kwa miezi mitatu hadi mwakani.


Akichonga na safu hii juzikati, jijini Dar akiwa njiani kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar ambako aliondoka na Ndege ya Scandinavia Airways, Lucy alisema:


“Ni kweli nasafiri, nakwenda Denmark kucheza filamu. Nitakuwa kule kuanzia Oktoba hii, Novemba, Desemba na Januari.”


Miezi ya hivi karibuni, Lucy amekuwa akienda kufanya ‘shooting’ ya filamu nje ya nchi. Katikati ya mwaka huu, alikwenda Ghana, Nigeria na baadaye Burundi.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!