Friday, October 5, 2012

MAANDALIZI YA FIESTA YAMEKAMILIKA NA RICK ROSS ATATUA MUDA WOWOTE JIONI HII

Rick Ross anatarajia kutua leo jijini Dar es Salaam tayari kwa show yake ya kesho ya Fiesta kwenye uwanja wa Leaders Club.

Haijulikani rasmi ataingia muda gani lakini anategemea kuingia mida ya jioni.

Masaa Kadhaa yaliyopita kupitia Twitter aliandika kuwa yupo Amsterdam na kutweet kwa kuandika “Approved #Dicedpineapples final Video edit on flight to #Africa .Coming soon!!”

“KLM airlines need 1st 48 on they’re tv’s for me. #Africa.” 
 
Katika maeneo ya kuuzia tiketi hizo zinazouzwa kwa shilingi elfu 20, wapenzi wa burudani wameonekana kwa wingi kununua tiketi zao tayari kwa kushuhusia show hiyo ya kihistoria.

Hizi ni miongoni mwa picha za matayarisho ya stage na maeneo ya kukalia watazamaji.
 

 ==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!