Wednesday, October 17, 2012

MBUNGE WA MBEYA AAMUA KUJIKITA KATIKA BIASHARA YA POMBE.
Wanywaji wa pombe nchini wategemee kupata ‘kick’ ya nguvu kutoka kwenye kilevi kipya kinachoanzishwa na mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi.

Kilevi hicho kinaitwa ‘Deiwaka Gin’ – The spirit of Tanzania.
Sugu ameivunja habari hiyo jana kupitia ukurasa wake wa Facebook kwa kuweka logo ya kilevi hicho na kuandika, “COMING SOON TO A BAR NEAR U.”

Wazo hilo la kuanzisha kilevi linaashiria kuwa mipango yake ya kuingia kwenye bishara ya radio kama alivyokuwa akiwaza kwa muda mrefu limekufa rasmi ama ameliweka pending kwanza.

Pamoja na wazo hilo kuungwa mkono , wapo watu wenye hofu na biashara hiyo ya Sugu ambapo mmoja amesema, “Hii kwa vyapombe iko poa! Ila kwangu mimi naona ni katika harakati za kututoa katika reli na ku support ushetani.”

“Hofu yangu ni mapafu ya wapiga kura, nikiwaumiza lazima nguvu kazi itapungua,” alisema mwingine.

Unaizungumziaje idea hii ya biashara ya Sugu?
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!