Saturday, October 6, 2012

MCHINA ATIWA MBARONI KWA UTENGENEZAJI WA BIDHAA FEKI


KUFUATIA kushamiri kwa bidhaa feki Bongo, Jeshi la Polisi wa Kituo cha Buguruni, Dar limefanikiwa kumnasa kijana mmoja mwenye asili ya Kichina kwa tuhuma ya kutengezeza bidhaa hizo.

Mchina (jina halikupatikana)amedaiwa kutengeneza mabati feki na kuyagonga nembo ya Shirika la Viwango vya Ubora Tanzania (TBS) katika ghala lililopo Kiwalani Dar, ametiwa mbaroni huku waandishi wakishuhudia.

 Mbali na Mchina huyo, polisi pia  walimtia mbaroni mkalimani wa Mchina huyo aliyefahamika kwa jina la Lyimo na kuwafikisha wote wawili katika Kituo cha Polisi cha Buguruni kwa ajili  ya  mahojiano zaidi.

Waandishi walikuwepo wakati Mchina na mkalimani wake wakitupwa rumande baada ya kuhojiwa na uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukiwa unaendelea wakati ghala la Mchina huyo likiwa limepigwa kufuli.

 Kabla ya kumnasa Mchina huyo, polisi walifanya kazi ya ziada kumdhibiti kutokana na kutaka kurusha kareti alipokuwa akigoma kupelekwa kituoni lakini hata hivyo alitulizwa.

Walioshuhudia tukio hilo walilipongeza jeshi la polisi kwa kulishughulikia suala hilo la bidhaa feki na kuitaka serikali kuhakikisha kuwa sheria inachukua mkondo wake.

Gazeti la Risasi
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!