Thursday, October 25, 2012

MDOMO WAMPONZA CHAZ BABA.......NI BAADA YA KUTANGAZA KUMUOA LULU MICHAEL NA MAMBO KWENDA KOMBO

RAIS wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ yupo kwenye gogoro zito na wanawake aliozaa nao, mama Jack na mama Carina baada ya hivi karibuni kutangaza ndoa na staa wa filamu aliye gerezani, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Akiongea na mwandishi wa habari hii,  Chaz Baba alisema katika stori za magazetini kwa mwaka huu, ya kumuoa Lulu imemfikisha pabaya.

“Ilipotoka tu ile habari, wakanipigia simu kila mmoja kwa wakati wake, maswali mengi, nilijaribu kuwaweka sawa lakini hakuna aliyenisikiliza zaidi ya kunikatia simu,” alisema Chaz Baba.


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!