Monday, October 1, 2012

MDOMO WAMPONZA JACKLINE WOLPER NA KUYAFANYA MAISHA YAKE YAWE YA CHUMBANI

SIKU chache baada ya mwigizaji  Jacqueline Wolper Masawe kumlipua mchumba’ke, Abdallah Mtoro, ‘Dallas’ inadaiwa kuwa mwigizaji huyo anaishi kwa ‘machale’ akihofia kuuawa kutokana na ukweli wa maisha yao aliouanika gazetini.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Dallas hakufurahishwa na sentensi za Wolper ambazo alizielekeza kwake huku akidai amemdhalilisha aliposema kuwa jamaa huyo hana chake na anatembea na nguo zake katika gari ili muda wowote amkabidhi.

“Kusema kweli sasa hivi Wolper anaishi kama digidigi, haonekani hovyo kama zamani.Nadhani  anamuogopa mpenzi  wake maana  huenda akamfanyia  kitu  mbaya". kilisema chanzo chetu na  kuongeza.

"Kauli alizozitoa gazetini zilikuwa tata  sana na huenda zimemuuma  sana  mchumba  wake ambaye  alikuwa nimtu wake wa siku nyingi"
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!