Thursday, October 4, 2012

MKE WA MPIGA PICHA WA TBC ALIYEPIGWA NA MSANII WA BONGO MOVIE, RICHIE AZUNGUMZA NA CLOUDS FMMke wa mpiga picha wa kituo cha televisheni cha TBC1 aitwaye Moses amezungumza sababu zilizopelekea msanii wa Bongo Movies, Single Mtambalike aka Richie Richie kumpiga mume wake na kumjeruhi vibaya.

Kutokana na tukio hilo, Richie alishikiliwa na polisi lakini alifanikiwa kutoka siku ya Jumapili kwa dhamana baada ya wasanii wengine wa filamu kuimba msamaha familia ya Moses.


Akiongea na Clouds FM jana, mke wa Moses amesema Richie aliamua kumpiga mume wake kwa kile anachodai kuchukia baada ya kumuona akipiga picha za tukio la birthday ya msanii mwenzie ajulikanaye kwa jina maarufu la Spompa Pomba.

Ameeleza kuwa mume wake bado anaumwa kwa kuwa alivunjwa taya na hivyo kupelekea kufanyiwa upasuaji wa mdomo na kwamba anaweza kukaa hospitali kwa zaidi ya miezi miwili.

Nao wafanyakazi wa TBC1 wamekilaani kitendo hicho cha kupigwa mpiga picha wao ambaye alikuwa kazini.
Moses amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!