Monday, October 1, 2012

MSAANII WA BONGO MOVIE " SINGLE MTAMBALIKE ( RICHIE ) " AENDELEA KUSOTA RUMANDE...


BAADA ya kumpiga na kumjeruhi Mpigapicha wa Runinga ya Taifa ya TBC1, Moses Friday na kisha kujisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Mabatini, Kijitonyama jijini Dar, mwigizaji Single Mtambalike ‘Richie’  anajutia kitendo hicho ambacho kimemfanya aendelee kusota  rumande

Kwa mujibu wa msanii mmoja aliyeenda kumtembelea Richie kituoni hapo, alitonya kuwa msanii huyo anajutia kitendo alichokifanya baada ya polisi kumzuia rumande mpaka Moses atakapopona.

Hata hivyo, jitihada za baadhi ya wasanii kwenda kwa ndugu wa Moses kumuombea msamaha Richie ziligonga mwamba baada ya familia ya mpigapicha huyo, kukataa msamaha huo kwa madai kwamba hali ya ndugu yao bado hairidhishi.

Wakati huohuo, baadhi ya wafanyakazi wa TBC1, wamekilaani kitendo alichokifanya msanii huyo kwa kumuumiza vibaya Moses kisa kikiwa ni kupigwa picha tu kitu ambacho ni cha kawaida kwa msanii kama yeye.

Habari za uhakika ni kwamba Moses amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili na kwa jinsi alivyoumia inabidi aagiziwe ‘pleti’ za kuunganisha taya kutoka nchini Kenya.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!