Monday, October 8, 2012

MSANII WA BONGO MOVIE AAMUA KUJICHORA TATOO KATIKA MAKALIO YAKE
MSANII ndani ya tasnia ya filamu na tamthilia za kibongo Rayuu amezidi kujichora tattoo kwenye mwili wake ambapo sasa aamua kuchora kiunoni na sehemu 
nyingine nyeti. 

Mtandao huu  baada ya kusikia taarifa hizo kutoka kwa rafiki yake kipenzi kuwa msanii huyo amezidi kujichafua mwili kwa kujichora ndipo ulipoamua kumtafuta ili kupata ukweli wa ishu hiyo na alipopatikana alifunguka kuwa ni kweli lakini zote alizochora hazina ubaya wowote.

Rayuu
alisema kuwa amechora michoro hiyo sehemu nyingi za mwili wake kuanzia kiunoni, shingoni, kwenye maziwa, makalio na mapaja na alidai kuwa anajisikia furaha kuwa na tattoo hizo kwani hajafanya kwa kushawishiwa na mtu.


Alidai kuwa hata hivyo kati ya michoro hiyo aliouweka kiunoni unasomeka jina lake la 
‘Rayuu’ na mengine ni ya aina mbalimbali, “tattoo nazipenda sana lakini kati ya zote hii ya kiunoni naipenda kuliko zote ingawa aliyenichora aliikosea kidogo,” alisema.==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!