Tuesday, October 9, 2012

"ACHANA NA H. BABA MAANA HANA UELEKEO WA KIMAISHA".......HUU NI UJUMBE WA SHILOLE KWA FROLA MVUNGI


Frola Mvungi

BAADA ya kutofautiana na kuwekeana bifu kwa muda mrefu, sasa msanii anayeshika kazi ndani ya bongo Shilole, ameibuka upya na kudai kuwa rafiki yake Frola Mvungi anaendelea kuwa maskini kwa sababu hataki kuachana na H-Baba ambaye hana muelekeo wowote wa maisha ingawa anafanya muziki na filamu.

Shilole
na Frola Mvungi walikuwa wanaishi kwenye chumba kimoja cha kupanga awali kabisa na inadaiwa kuwa Frola ndiye aliyempokea Shilole miaka kadhaa nyuma lakini walikuja kutofautiana na ndipo Mvungi alipoamua kuchukua hatua ya kumfukuza mwanadada huyo.

Shilole
anadai kuwa walikuwa wakifanya misheshe wote lakini kadri siku zinavyozidi kwenda hakuna kitu ambacho mwenzake anakipata zaidi ya kukaa na kumtengemea H-Baba, kitu amacho anaamini tabia hiyo itakuja kumtokee puani mwisho wa siku.

Shilole

Alidai kuwa zipo filamu kadhaa ambazo wamecheza pamoja lakini haoni mafanikio yoyote ambayo ameyapata na anahisi kila ishu anayopata huwa haifanyii kazi bila kauli ya mpenzi wake huyo ambaye anamuona kama Mungu wake kwa maisha haya ya sasa.


“Kila mtu ana maisha yake, yeye kama anahitaji kusonga mbele angeachana na huyo mpenzi wake kwani muda wote huo hakuna kitu Frola ambacho anaweza kusema anajivunia tangu alipoanzisha mahusiano na H-Baba,
alisema.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!