Tuesday, October 2, 2012

"NILIOLEWA NA KUACHIKA NDANI YA SIKU NNE.....KWA SASA SIKO TAYARI KUOLEWA TENA".....SKAINA


MIEZI kadhaa baada ya kuvunjika kwa ndoa yake iliyodumu kwa  siku nne, mwanadada  kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ ameiambia mpekuzi  kuwa kwa sasa hayupo tayari kuolewa tena kama ilivyokuwa mwanzo bali kuolewa kwake kutachukua muda mrefu.

Skaina alisema hana wazo la kuolewa ila akitokea mwanaume anayejitambua na ambaye anataka kuoa kweli, ataolewa, lakini siyo kama ilivyokuwa mwanzo kwani alipata mchumba kwa muda mfupi na kuolewa  jambo ambalo halikuwa na mafanikio.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!