Wednesday, October 24, 2012

"WANAWAKE NATURAL WAMEKWISHA SIKU HIZI"....BONGO5


Na Bongo5:

Ni jambo lisilofikirika kwa urahisi katika vichwa vya watu wengi lakini mdadisi mmoja wa mambo juzi alinipa mtihani ambao nimebidi nijaribu kuwashirikisha ninyi wadau wetu, maana baada ya mdadisi huyo kuuliza swali mbele ya washkaji zake mimi nikiwemo, mjadala ukawa mkali sana kiasi cha muafaka kutopatikana kwa urahisi.

Swali alilohusisha mdadisi huyo(jina kapuni) ni Je siku hizi wanawake natural wamepotea? 

Mada ilianza hivi baada ya hapo kila aina ya majibu yalitoka na muda mwingine kuamsha taharuki, kila mtu akivutia katika pointi ama maoni yake.

Baada ya tafakari ndefu siku ya jana nikapata baadhi ya mambo ambayo naomba wasomaji wetu tuchangie kadiri tuwezavyo. Katika tafakuri yangu nilianza kuwachambua akina dada ambao tupo nao karibu.
Nikianza na nilivyowajua baadhi yao wakati wakiwa bado vijana wadogo, nikagundua kuna tofauti kubwa sana kati ya wakati ule na leo. Moja ya mabadiliko ni pamoja na rangi na baadhi ya viungo katika ya miili yao.

Tofauti hizo zinaanzia kichwani. Nywele zilizokuwapo kichwani mwao wakati ule sio nywele za sasa. Sasa kuna ma weaving, Less wigs, Rasta za kusukia, nywele za ki Brazilian na ki Hindi na kila aina ya vikorombwezo. Ukishuka chini kidogo karibu na jicho nyusi za sasa nazo hazipo tena. 

Sijui sababu kubwa iliyopelekea jambo hili kutokea na badala yake mistari yenye rangi ime replace nyusi za dada zetu. Usishangae kuona kope nyekundu, blue ama rangi ya dhahabu.
Na katika eneo hilo hilo kope za dada zetu siku hizi nazo zinachezewa na kuongezewa mapambo. Ajabu na kweli.tukiwa bado tupo eneo hilo hilo la kichwa tunashuka chini kidogo ni nadra kumkuta msichana siku hizi ajapaka lipshine za aina mbali mbali ili kuongeza mvuto katika lips zake.

Ukitoka hapo unabaki na kichwa chenyewe hapo sasa ndipo uhalisia kwa asilimia kubwa unapokuwa haupo. Rangi ya kichwa, shingo, na sehemu nyingine za mwili kama mikono na miguu zinapishana kweli kweli. 

Siku hizi ni lazima ujichubue ama uondokane na rangi yako uliyozaliwa nayo na uonekane na muonekano wa Carolite ama vipodozi aina ya lotion. 

Mtihani huo hata wanaume wamefeli pia siku hizi.
Ukiondokana na eneo la kichwa unashuka kwenye fahari ya kwanza ya mwanamke ambayo ni maziwa. Siku hizi wanasema kuna hadi Brazilia za kukuza matiti. 

Suala hili limekuwa likiripotiwa katika magazeti ya udaku kwamba dada zetu wanafanya kila aina ya jitihada alimradi wawe na maziwa makubwa. Sijui maana yake ni nini hapo.
Ukitoka eneo hilo unashuka kwenye fahari ya pili ya mwanamke hapo nazungumzia hips na makalio. Sasa hapo pia hali imekuwa tofauti maana mchina ndiye anyehusika sana nadhani kwa eneo hili sitaongelea sana kwani matokeo yake yapo wazi na kwa sababu mjadala wa suala hilo umekuwa wazi sana.
Kikubwa ambacho kinaonekana kwenye makala hii ni kwamba dada wa kike au mwanamke wa leo anatawaliwa na vikorombwezo vingi ku boost image, mwonekano ama mvuto wake kiasi kwamba ukikutana na dada zetu unashangaa kimetokea nini. Hata kucha sasa kuna acrylic nails sasa hapo ana nini cha kwake maana kila mahali ana modification?

Hapa naomba nibalansi hii makala hatusemi kuwa mtu kupaka mafuta na kushine ama kung’aa ni kuondokana na uhalisia. La hasha bali mwanamke wa leo mathalani kuna sherehe basi tegemea kukutana vibweka. Mfano wa harusi, ama kuna tukio la kijamii kama Miss Tanzania basi kazi kubwa katika siku hiyo inafanyika saluni.

Na huko ndipo gereji za kuondoa ama kubadilisha uhalisia wa dada zetu, maana spea na spana zote za kufanyia kazi hiyo zipo huko. Mi ni kama yule mdadisi ambaye anasema ame miss mwanamke natural wa kitanzania ya na si photocopy ya Rihanna ama Nicki Minaj.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!