Thursday, October 4, 2012

"NILIVUNJA NDOA YA LUTEN KALAMA KWA SABABU YEYE NDO ALINITOA BIKIRA".......ISABELA


IMEBAINIKA kuwa ile ndoa ya mwanamuziki wa kitambo ndani ya Bongo Fleva, Luten Kalama ilivunjika miaka mingi iliyopita chanzo kikitajwa ni mpenzi wake wa sasa Isabela Mpanda.


Kwa mujibu wa chanzo makini, ndoa ya Kalama na mkewe Shufaa iliyofungwa mwaka 1998 haikuwa na uhai kwani miaka michache baadaye, walitofautina ingawa hawakuweka wazi ugomvi wao.


 Kwa mujibu wa chanzo hicho, wanandoa hao walikuwa wakigombana mara kwa mara huku mwigizaji, Isabela akitajwa kuwa chanzo cha kuvunjika.


Mpekuzi wetu alimtafuta Kalama ili kujua uhai wa ndoa yao ambapo alikiri kuvunjika na kusema kwa sasa yupo na Isabela.


Kwa upande wa Isabela alipoulizwa kuhusika kuivunja ndoa hiyo, alisema:


“Heh! Kalama na mimi damdam. Chezea Kalama wewe, kanitoa usichana ati Kwa hiyo mlitaka  mimi  ndo niachike. Siwezi kumuacha miaka mia nane.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!