Tuesday, October 2, 2012

NDOTO YA JACK WOLPER KUTEMBELEA MAGARI YA KIFAHARI IMEFUTIKA RASIMI BAADA YA "KUTEMWA" NA MPENZI WAKE DALLAS..SINTAH AMPA POLEWAKATI hali ya kimaisha ikiwa tete kwa msanii anayefunika kwa urembo bongo movie Jackline Wolper, ambaye alikuwa akitembelea magari ya kifahari kila kukicha, sasa anachoambulia ni pole kwani shosti yake wa karibu Sintah, amedai kuwa kuachana kwao na ‘Dallas’ kutamfanya Wolper ayakumbuke magari yake ya zamani kama vile Noah.

Wolper
ni msanii wa kwanza bongo kutembelea magari ya kifahari tena baada ya kumpata jamaa huyo lakini awali kabisa alikuwa akitembelea Noah, na inadaiwa kuwa sasa atakuwa akiyaona kwa macho watu wakiendesha kwani Dallas amechukua funguo zote za magari yake.

Ishu hii ikiwa inashika kasi mjini huku watu wakiwa macho juu kutaka kuona nini kinachoendelea kwa
Wolper, Sintah hakusita kudai kuwa mara nyingi mapenzi ya kwenye magazeti huwa hayadumu kwani awali kabisa Wolper alijitangazia kuwa hawawezi kuachana na Dallas huku akisahau kuwa kuna wabaya wake wanaomtazama.

Akiongea na Mpekuzi, Sintah
alidai kuwa kwa njisi anavyo mfahamu Wolper haoni kama yeye atakuwa ndiye chanzo cha kuachana kwao kwani kuna wabaya wake ambao wamejaa fitna, lakini kwa upande wake anampa pole ili sasa ajipange na kuacha tabia ya kuishi mjini kwa kuwatengemea wanaume, hasa wale anaokutana nao mjini.

“Kuachana ni kawaida miaka ya sasa kwanza kama huna hela huwezi kutembea na staa bongo na Dallas alimpenda Wolper kwa sababu ni staa, lakini sioni kama kuna tatizo wao kuachana kwani wamekutana mjini na wanaachana kimjini,”
alidai.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!