Tuesday, October 2, 2012

"BORA NIUGUE MARALIA KULIKO UGONJWA WA MAPENZI MAANA HUNICHUKUA MUDA KUPONA".....JACK WA MAISHA PLUSMwanadada  aliyepata jina kupitia Shindano la Maisha Plus Season II, Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’ ambaye kwa sasa anafurukuta kwenye filamu za Kibongo amefunguka kuwa ni mgonjwa kwenye mapenzi na kama ikitokea akasalitiwa anaweza hata kulazwa hospitali akiwa hajitambui.

Jack aliiambia mpekuzi  kuwa mara nyingi akimpenda mwanaume humpenda kisawasawa na pale anapotokea kusalitiwa anakuwa mgonjwa na hata chakula kinakuwa ni kigumu kupita katika koo kutokana na kuzimika katika dimbwi la mapenzi kupita maelezo.

  “Kwa kweli bora niugue malaria coz najua nitakunywa dawa then nitapona lakini sitaki kabisa kuugua ugonjwa wa mapenzi unanifanya nakonda na huwa inanichukua muda mrefu kupona.”..
JACK
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!