Thursday, October 25, 2012

PENZI LA SHILOLE NA BARNABA LAREJEA KWA SIRI


KUNA tetesi kuwa, penzi lililokuwa limekufa kati ya mwigizaji wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Mbongo Fleva, Elias Barnaba limerejea kwa ari, nguvu na kasi mpya.


“Hivi karibuni wawili hao walionekana chobingo, Mbeya kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta na hata Dar pale Leaders Club, walikuwa "close" nyuma ya jukwaa katika gari la Shilole,” alisema mpashaji wetu.


Mwanahabari wetu aliwatafuta hewani wote, lakini Shilole ndiye aliyepatikana, akafunguka:

“Kwani tatizo lipo wapi tukirudiana? Mbona hamuwashangai akina Chris Brown na Rihanna? Mapenzi ni upofu acheni hizo,” alisema Shilole. 

 
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!