Wednesday, October 10, 2012

"JAPOKUWA ROSE MUHANDO ANAKATA SANA MAUNO, MIMI SIONI KOSA LAKE"......HAYA NI MANENO YA PRODUCER WA ROSE MUHANDO


Wasanii wa Injili hapa nchini  wamekuwa  wakimkosoa Rose Muhando kutokana  na  staili ya nyimbo zake  na uchezaji wake.....

Wasanii  hao wamekuwa  wakidai kuwa Rose Muhando  amekuwa akicheza mno na kukata  mauno sana  hali ambayo wanadhani kuwa hafikishi ujumbe  katika hali inayotakiwa

Pamoja  na  shutuma hizo, Wasanii hao wanadai kuwa Rose amekuwa akifikisha ujumbe  mkali sana kwa jamii bila kujali mapokeo yake.......

Lawama hizo zimemfanya  producer wa Rose muhando afunguke  na kudai kuwa  yeye  binafsi   haoni  kama  kucheza  sana  ni tatizo  na  kuongeza kuwa  mwimbaji yeyote  anajukumu la kuionya  na  kuielimisha jamii  kama  afanyavyo Rose Muhano.....

"Rose mhando  hana kosa lolote.kama  anacheza sana basi mwacheni maana hiyo ndo stail ya nyimbo zake'producer
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!