Friday, October 26, 2012

SALHA ISRAEL AVAMIWA USIKU.....GARI LAKE LANUSURIKA KUBEBWA


WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi juzikati walivamia nyumbani kwa Miss Tanzania 2011, Salha Israel maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar na kufanya jaribio la wizi.
Akizungumza na mwandishi wetu, Salha alisema tukio hilo lilijiri hivi karibuni mishale ya saa 8:00 usiku ambapo watu hao wasiofahamika waliruka ukuta na kutaka kufanya uhalifu lakini walishitukiwa kabla ya kutekeleza mpango huo.

“Sijui niseme ni wezi au majambazi ila ilikuwa saa 8 usiku, watu hao waliruka ukuta wakaingia ndani. Hutujui kama walitaka kuondoka na gari au kuiba vitu vilivyokuwemo ndani yake lakini walivunja kioo cha mbele.

“Kwa bahati tulisikia vurugu zao na kabla ya kuiba chochote, tuliwakurupusha na ndipo walipokimbia,” alisema Salha.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!