Tuesday, October 2, 2012

SHILOLE NA SNURA WAPIGANA VIJEMBE KUHUSU VIUNO VYAO


WAKATI mashabiki wengi wakiwa na maswali mengi juu ya wasani wawili wanaofanya filamu na muziki, Shilole na Snura, kuwa wanaweza kushindana kutokana na kazi zao kufanana, mtandao huo uliwatafuta warembo hao ambapo wote walidai kuwa hakuna anayetaka kuwa kama mwingine na kutambiana kuwa wanaojua ni mashabiki.

Katika baadhi ya shoo za
Snura na kati ya vitu ambavyo alikuwa anavifanya vinaendana na Shilole ikiwemo kukatika viuno pamoja na wacheza show wake kuvaa nguo zinazoendana na wale wa Shilole.

Snura
alidai kuwa hata kama Shilole ameanza kufanya muziki kabla yake na kuwika zaidi lakini yeye alianza kazi hiyo kitambo ingawa hakutaka kuingia mapema kwani alijikita kwanza kwenye filamu pekee.Snura akimwaga mauno stejini kwenye moja ya shoo zake


Alisema kuwa kiwango chake hakina mfano hivyo anaamini watu wanaojua ubora wake ni mashabiki wake pekee na si kuchambuliwa na mtu ambaye anapata umaarufu kupitia magazeti.


“Nafanya muziki si kwa sababu ya kushindana na mtu sipo kwenye game kwa lengo la kushindana na Shilole, kazi zangu zinalengo la kuburudisha mashabiki na mimi mwenyewe kufika mbali zaidi”
alisema Snura.Shilole kwa stage


Naye
Shilole, alidai kuwa hawezi kutambiana na mtu ambaye hana ngoma inayojulikana ambapo aliongeza kuwa hata mashabiki wake wanajua kiwango chake kuanzia kwenye filamu hadi upande huo wa muziki.

“Snura hana chochote kwangu na watu wanaosema kuwa anafanana na mimi kwenye game hao si wafuatiliaji, kiwango changu hakina mfano na naweza kusema hata wale ambao wameanza fani hii kitambo kwangu watasuburi sana,
alisema Shilole.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!