Wednesday, October 31, 2012

SUMALEE AIBIWA GARI LAKE


Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri haina shaka kuwa utakuwa unakumbuka stori iliyochukua nafasi kwenye kipindi cha XXL siku chache zilizopita juu ya nyota wa songi la 'Hakunaga' Suma Lee kupata ajari wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya kupiga shoo.

Taarifa kutoka Coco Beach zinasomeka kuwa nyota huyo mzaliwa wa mkoa wa Tanga ameibiwa ndinga yake hiyo aina ya Land Cruiser VX mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipokuwa kwenye mapumziko ya wikiend katika ufukwe wa bahari ya hindi.


"haikuwa siku nzuri kwangu, nimeibiwa gari na watu ambao nahisi walikuwa wanaifuatilia kwa siku nyingi maana hata wakati wanaiba watu waliokuwa karibu waliniambia kuwa watu hao hawakuvunja wala kuharibu chochote..... walichokifanya ni kufungua mlango kama ambavyo mimi huwa nafanya na kuwasha gari kisha kuondoka nalo kama la kwao" alisema Suma


Akiendelea zaidi suma alisema kuwa kwa kuwa suala liko polisi hawezi kuzungumza sana ila ana uhakika gari yake ataipata tu kwani anafahamu watu wengi wanouza vifa avya magari kariakoo labda  watu hao waaamue  kulifugia kuku.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!