Saturday, October 6, 2012

“TAARAB HUBADILIKA KULINGANA NA MAHITAJI YA MASHABIKI” – ISHA MASHAUZI

MUIMBAJI wa muziki wa taarabu bongo ambaye pia ni mmiliki wa kundi la Mashauzi Classic, Isha Mashauzi, ameuambia mtandao huu kuwa muziki huo sasa umebadilika tofauti na zamani lakini wanaofanya hadi ubadilike ni mashabiki kwani wanalazimika kuwapa kile wanachokihitaji.

Awali muziki wa huo ulikuwa ukiimbwa kwa staili moja ya kukaa chini na ulikuwa hauna wacheza viduku kama ilivyo sasa, kitu ambacho wadau wengi wanaoujua muziki huo ulikotoka wanasikitika kuona unafanywa kama bongo fleva.


Isha alizungumza kiundani kwa kudai kuwa mashabiki wao huwa wanawapa kile wanachokihitaji kwani bila wao hawezi kufanya muziki huo. Alisema kuwa anaelewa awali muziki huo ulikuwaje lakini mambo yanaenda na kubandilika ingawa kwa upande wake muziki wa sasa anaona unalipa zaidi kutokana na staili ambazo wanakuja nazo za kibunifu tofauti na zamani.


“Zamani wakati muzikai huo unashika kasi kulikuwa hamna wacheza viduku kama sasa lakini miaka inabandilika kitu cha jana hakiwezi kufanana na leo, hivyo naweza kusemam kwamba kila kitu huwa kinabandilika kutokana na mahitaji ya watu,”
alisema.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!