Saturday, October 13, 2012

T.I.D AJIPANGA KUTOKA NA "KIUNO" CHAKE.....

MSANII mkongwe ndani ya game la mziki TID, au unaweza kumuita sauti ya pesa, ameuambia mtandao huu  kuwa baada ya ngoma yake ya ‘Kiuno’ kufanya vizuri sasa anatarajia kuachia albamu ambayo itakuwa na nyimbo nane huku kukiwa na kazi nyingine ambazo hakuwahi kuziachia.

Hata hivyo alisema kuwa jina la albamu hiyo imebebwa na goma yake ya
‘Kiuno’, ambapo ngoma nyingine zitakavyokuwepo ndani ni pamoja na ‘Raha’, ‘Check Me’, na nyingine kibao kwani alishindwa kutaja majina kwa madai kuwa wasanii wa sasa wana tabia ya kuiba majina na kuyafanyia kazi.

Aliongeza kuwa albamu imeshakamilika na kitu kinachosubiriwa sasa ni uzinduzi kwani, anaamini ujio huu utamfanya aweze kurudi kwenye chati kama ilivyokuwa zamani.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!