Tuesday, October 23, 2012

T.I.D AKITETEA "KIUNO" CHAKE


Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa muimbaji Khalid Mohamed aka Top in Dar amecopy wimbo wa Shayman uitwao Fendela Fenduze na kuupa jina la "KIUNO". Tumepata fursa ya kuzilinganisha nyimbo hizo. 

Tofauti na shutuma hizo tumegundua hakuna mfanano wowote wa nyimbo hizo na kuamua kumpigia simu TID kumuuliza analizungumziaje suala hilo.

“Mimi naona tu kuna watu ambao wanataka kuniangusha. Kwasababu wameona muziki wangu unakua vizuri kwahiyo hawataki nipate advantage wananiharibia lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye amemcopy huyo jamaa wala simjui toka nilivyozaliwa,amesema TID.

“Sababu mimi sijafanya kosa lolote mimi nitakatu kimya, nitaangalia.”

Hiyo sio mara ya kwanza kwa TID kuzushiwa kucopy wimbo wa msanii mwingine kwani aliwahi pia kuingia kwenye shutuma ya kucopy wimbo wa Irmãos Verdades uitwao Amar-te assim ambao kweli ulifanana kwa asilimia kubwa.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!