Saturday, October 13, 2012

TIKO HASSAN ADATA NA PENZI LA MUME WA MTU


MSANII wa filamu ambaye anadili na muziki pia, Tiko Hassan amemtungia wimbo mpenzi wake wa sasa ambaye ni mume wa mtu  kwa lengo la kupalilia penzi.

Tiko aliliambia mekuzi kuwa ni kweli amekuwa kwenye uhusiano na mume wa mtu ambaye anampenda na kumthamini na katika kulilinda penzi ameamua kutunga wimbo kusifu yale anayopata kutoka kwa mwanaume huyo.


 “Ni mwanaume anayeonesha mapenzi ya dhati kwangu, ananijali na kunithamini sana   ndiyo maana nimeona nioneshe hisia zangu kupitia wimbo nilioupa jina la Mimi na Wewe,” alisema Tiko.


Amesema watu wanaweza kumshangaa kwa kunga’nga’nia penzi la mume wa mtu lakini akadai haoni hatari kwa kuwa anapata anachokitaka.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!