Saturday, October 13, 2012

"WANAWAKE TUNA HAKI SAWA YA KUTEMBEA VIFUA WAZI KAMA WANAUME"...MOIRAMsichana anayeitwa Moira Johnston ameonekana akitembea matiti nje, bila blouse wala sidiria (topless) katika jiji la New York, Marekani. 
 
Moira amethibitisha kwamba anatembea matiti nje kuikumbusha jamii kwamba wanawake wana haki ya kutembea vifua wazi kama wanaume.
 “Natembea topless kuhamasisha hiyo ni halali kwa mwanamke kuwa topless mahali popote ambapo wanaume wanaweza kuwepo bila kuvaa mashati.” MOIRA

 Moria aliendelea, “Nimekuwa natembea topless kwa muda wa wiki kadhaa sasa. Nimepata maoni mnyanganyiko.” 
Alisema kwamba watu wengi wako poa ila kuna wengine wanashangaa sababu hawajazoea kuona wanawake wakitembea matiti nje. Moira anapenda kubadilisha hilo ili iwe kawaida kwa wanawake kutembea matiti nje.


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!