Saturday, October 27, 2012

"NINA UHURU WA KUTOA PENZI KWA MTU YEYOTE NINAYEMPENDA.....WANAODAI NATEMBEA NA WAUME ZA WATU NI WANAFIKI".......AGNESS MASOGANGE


MWANADADA anayejipatia umaarufu kupitia video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya,  Agness Masogange, ameuambia mtandao huu kuwa hatumii mwili wake kama chombo cha kuwakamata wanaume bali hutoa penzi lake kwa yule anayempenda na ishu zinazozungumzwa mitaani kuwa anaongoza kwa kuiba wanaume za watu si kweli na wanaodai hivyo hawamtakii mema.

Mwandishi wetu alizungumza na mwanadada huyo juu ya ishu kadhaa zinazongumzwa juu yake, ndipo alipofunguka kuwa hatumia uzuri wake au umbo lake kama njia ya kuwavuta wanaume kwani angeamua kufanya hivyo basi angekuwa na wanaume wengi sana.

“Mwili wangu si chombo cha kuwakamata wanaume na hao watu wanaosema kuwa naongoza kwa kutembea na wanaume za watu ni wale wenye nia ya kunichafua kwani mi si demu wa hivyo,” alidai

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!